• HABARI MPYA

  Jumatano, Novemba 06, 2019

  SALIBOKO APIGA HAT TRICK LIPULI YAITANDIKA SINGIDA UNITED 5-1, COASTAL YACHAPWA TENA NYUMBANI

  Na Mwandishi Wetu, IRINGA
  TIMU ya Lipuli FC ya Iringa imeweka rekodi ya ushindi mkubwa katika msimu huu wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya leo kuichapa Singida United 5-1 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Samora mjini Iringa.
  Mshambuliaji Daruwesh Saliboko amefunga mabao matatu peke yake dakika za 43, 72 na 87, huku mengine mawili yakifungwa na mshambuliaji mwenzake, Paul Nonga dakika ya 23 na 58, wakati bao pekee la SIngida United limefungwa Jonathan Daka dakika ya 52.
  Kwa ushindi huo, Lipuli FC inafikisha pointi 18 baada ya kucheza mechi 10 na kupanda hadi nafasi ya pilim nyuma ya mabingwa watetezi, Simba SC wenye pointi 21 za mechi nane, wakati Singida United inaendelea kushika mkia katika ligi ya timu 20 ikiwa na pointi nne za mechi 11.
  Daruwesh Saliboko akiwa na mpira wake baada ya kukabidhiwa kufuatia kupiga hat trick leo

  Mechi ya Ligi Kuu leo, bao pekee la Awadh Juma dakika ya 66 limeipa ushindi wa 1-0 Mtibwa Sugar dhidi ya Mwadui FC Uwanja wa CCM Gairo, nje kidogo ya Jiji la Morogoro.
  Polisi Tanzania wakapoteza mechi ya kwanza nyumbani baada ya kuchapwa 1-0 na Mbao FC, bao pekee la mshambuliaji Waziri Junior dakika ya 61.
  Coastal Union ikapoteza mechi ya pili mfululizo nyumbani baada ya kupigwa 1-0 na Alliance FC ya Mwanza bao pekee la Geofrey Luseke dakika ya 32, wakati JKT Tanzania ikashinda 1-0 nyumbani dhidi ya Mbeya City, bao pekee la Adam Adam dakika ya 22 Uwanja wa Meja Isamuhyo, Mbweni Jijini Dar es Salaam.
  Na Namungo FC ikaendelea kufanya vizuri nyumbani baada ya kuichapa Ruvu Shooting 2-1 Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi. Mabao ya Namungo yamefungwa na Nzigamasabo Steve dakika ya 45 na Kelvin John dakika ya 53 huku la Ruvu likifungwa na Sadat Mohamed dakika ya 48.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SALIBOKO APIGA HAT TRICK LIPULI YAITANDIKA SINGIDA UNITED 5-1, COASTAL YACHAPWA TENA NYUMBANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top