• HABARI MPYA

  Sunday, November 24, 2019

  SAMATTA AINGIA ’30 BORA’ TUZO YA MWANASOKA BORA, WAMO PIA SALAH, MANE NA MAHREZ

  Na Mwandishi Wetu, CAIRO
  NAHODHA wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta amejumuishwa kwenye orodha ya awali ya wachezaji 30 kuwania tuzo ya Mwanasoka Bora Afrika ambayo itatolewa Jumanne ya Januari 7 mwakani Citadel Azure, Hurghada nchini Misri.
  Samatta anayechezea KRC Genk ya Ubelgiji, ameingia tena kwenye kinyang’anyiro cha tuzo hiyo baada ya kuiwezesha Genk kutwaa ubingwa wa Ubelgiji, huku naye akiwa mfungaji Bora.
  Na anachuana na Mmisri, Mohamed Salah, Msenegal Sadio Mane, Mguinea Naby Keita wote wa Liverpool, Mgabon Pierre-Emerick Aubameyang, Waivory Coast Nicolas Pepe wote wa Arsenal, Wilfried Zaha wa Crystal Palace, Mualgeria Riyad Mahrez wa Manchester City, Mnigeria Wilfred Ndidi wa Leicester City na Mghana Thomas Teye Partey wa Atletico Madrid.

  Wengine ni Jordan Ayew (Ghana na Crystal Palace), Kalidou Koulibaly (Senegal na Napoli), Kodjo Fo Doh Laba (Togo na Al Ain), André Onana (Cameroon na Ajax), Baghdad Bounedjah (Algeria& Al-Sadd), Carolus Andriamatsinoro (Madagascar na Al Adalah), Denis Onyango (Uganda na Mamelodi Sundowns), Eric Maxim Choupo-Moting (Cameroon na Paris Saint-Germain) na Ferjani Sassi (Tunisia na Zamalek).
  Wamo pia Mahmoud Hassan ‘Trezeguet’ (Misri na Aston Villa), Achraf Hakimi (Morocco na Borussia Dortmund), Hakim Ziyech (Morocco na Ajax), Idrissa Gueye (Senegal & Paris Saint-Germain), Ismail Bennacer (Algeria na AC Milan), Moussa Marega (Mali na Porto), Odion Ighalo (Nigeria na Shanghai Shenhua), Percy Tau (Afrika Kusini & Club Brugge), Taha Yassine Khenissi (Tunisia na Esperance), Victor Osimhen (Nigeria na Lille) na Youcef Belaili (Algeria & Ahli Jeddah).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA AINGIA ’30 BORA’ TUZO YA MWANASOKA BORA, WAMO PIA SALAH, MANE NA MAHREZ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top