• HABARI MPYA

  Jumapili, Novemba 10, 2019

  LIVERPOOL YAICHAPA MA CITY 3-1 NA KUJITANUA KILELENI

  Sadio Mane (kulia) akishangilia na beki Virgil Van Dijk baada ya kuifungia Liverpool bao la tatu dakika ya 51 katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Manchester City kwenye Ligi Kuu ya England Uwanja wa Anfield leo. Mabao mengine ya Liverpool yamefungwa na Fabinho dakika ya 6 na Mohamed Salah dakika ya 13, wakati la Man City limefungwa na Bernardo Silva dakika ya 78. Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 34 baada ya kucheza mechi 12 na sasa inawazidi pointi tisa mabingwa watetezi, Manchester City ambao wanaporomoka hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England wakizidiwa pointi moja na zote Leicester City ya pili na Chelsea ya tatu   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YAICHAPA MA CITY 3-1 NA KUJITANUA KILELENI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top