• HABARI MPYA

  Alhamisi, Novemba 07, 2019

  RODRYGO APIGA HAT TRICK REAL MADRID YAICHAPA GALATASARAY 6-0

  Mshambuliaji kinda Mbrazil, Rodrygo Silva de Goes akishangilia baada ya kuifungia Real Madrid mabao matatu dakika ya nne, saba na 90 na ushei katika ushindi wa 6-0 dhidi ya Galatasaray kwenye mchezo wa Kundi A Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa Jumatano Uwanja wa Bernabeu. Mabao mengine ya Real yamefungwa na Sergio Ramos kwa penalti dakika ya 14, Karim Benzema dakika ya 45 na 81 na kwa ushindi huo, timu ya kocha Mfaransa Zinadine Zidane inafikisha pointi saba, ikiendelea kushika nafasi ya pili ikizidiwa pointi tano na vinara Paris Saint-Germain baada ya timu zote kucheza mechi nne 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: RODRYGO APIGA HAT TRICK REAL MADRID YAICHAPA GALATASARAY 6-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top