• HABARI MPYA

  Ijumaa, Novemba 08, 2019

  YANGA YAANZA ‘KUFAKAMIA VIPORO’, YAIPIGA NDANDA FC 1-0, KAGERA SUGAR YAICHAPA KMC 2-1 DAR

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  YANGA SC imepata ushindi wa ugenini katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuwachapa wenyeji, Ndanda FC 1-0 jioni ya leo Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara. 
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, nyota wa Rwanda Partrick Sibomana aliyefunga dakika ya 76 kwa shuti la mpira wa adhabu kutoka umbali wa mita 20.
  Refa Hance Mabena kutoka Tanga aliyekuwa anasaidiwa na Abdallah Rashid na Khalfan Sika wa Pwani aliamuru pigo hilo baada ya beki wa Ndanda FC, Aziz Sibo kuunawa mpira uliopigwa na Mrisho Ngassa nje kidogo ya boksi.
  Kwa ushindi huo, Yanga SC iliyokuwa inacheza mechi ya kwanza chini ya kocha mpya na wa muda, Charles Boniface Mkwasa kufuatia kundolewa kwa Mkongo Mwinyi Zahera, inafikisha pointi 10 katika mchezo wa tano, sawa na Azam FC ambayo hata hivyo imecheza mechi moja zaidi. 
  Mchezo mwingine wa Ligi Kuu leo, Kagera Sugar imeendelea kufanya vizuri baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, KMC Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.
  Mabao ya Kagera Sugar inayofundishwa na Nahodha wa zamani wa Taifa Stars, Mecky Mexime yamefungwa na viugno Awesu Awesu kwa penlati dakkika ya 25 na Peter Mwalyanzi dakika ya 48, wakati la KMC ya kocha Mganda, Jackson Mayanja limefungwa na Serge Nogues dakika ya 86.
  Kagera Sugar sasa ina pointi 20 katika mchezo wa 10, ikizidiwa pointi mbili tu mabingwa watetezi, Simba SC ambao wanaongoza kwa pointi zao 22 za mechi tisa.
  Kikosi cha Ndanda FC kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Aziz Sibo, Said Mbatty, Samuel Mauru, Paul Maona, Godfrey Malibiche, Omar Hassan, Abdul Suleiman, Kassim Mdoe, Omar Issa na Hussein Javu/Nassor Saleh dk64/Yassin Hamisi dk88.
  Yanga SC; Farouk Shikhalo, Juma Abdul, Jaffar Mohammed, Ally Mtoni ‘Sonso’, Kelvin Yondan, Papy Kabamba Tshishimbi, Deus Kaseke, Mapinduzi Balama, David Molinga, Raphael Daudi/Mrisho Ngassa dk66 na Patrick Sibomana/Issa Bigirimana dk90+1.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA YAANZA ‘KUFAKAMIA VIPORO’, YAIPIGA NDANDA FC 1-0, KAGERA SUGAR YAICHAPA KMC 2-1 DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top