• HABARI MPYA

    Sunday, November 24, 2019

    YANGA SC WALIPOVAA JEZI ZA STARS 1998 DHIDI YA ASEC MIMOSA

    Kikosi cha Yanga SC kabla ya mchezo wake wa kwanza wa Robo ya Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika Kundi B dhidi ya ASEC Mimosa ya Ivory Coast Novemba 8, mwaka 1998 Uwanja wa Taifa (sasa Uhuru) mjini Dar es Salaam uliomalizika kwa wageni kushinda 3-0. Kutoka kulia waliosimama ni Salvatory Edward, Banza Tshikala, Edibily Lunyamila, Manyika Peter, Idelphonce Amlima na Alphonce Modest. Waliochuchumaa kutoka kulia ni Monja Liseki, Mohammed Hussein ‘Mmachinga’, Shaaban Ramadhani, Mzee Abdallah ‘National’ na John Jacob Mwansasu. Yanga SC walilazimika kuvaa jezi za Taifa Stars kutokana na jezi zao pekee walizokuwa nazo (njano) kufanana na za wageni.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA SC WALIPOVAA JEZI ZA STARS 1998 DHIDI YA ASEC MIMOSA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top