// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); LUKAS PODOLSKI ATUA MILAN NA KUAHIDI MAKUBWA, MASHABIKI WAPAGAWA NAYE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE LUKAS PODOLSKI ATUA MILAN NA KUAHIDI MAKUBWA, MASHABIKI WAPAGAWA NAYE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, January 03, 2015

    LUKAS PODOLSKI ATUA MILAN NA KUAHIDI MAKUBWA, MASHABIKI WAPAGAWA NAYE

    MSHAMBULIAJI Lukas Podolski jana alipokewa kwa furaha na mashabiki baada ya kuwasili jiji la Milan kukamilisha uhamisho wa mkopo katika klabu ya Inter. 
    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 alikuwa amevalia skafu maarufu ya klabu hiyo ya rangi nyeusi na bluu wakati alipowasili Uwanja wa Ndege wa Linate mjini MIlan na akawasaini mashabiki wa timu hiyo.
    Podolski anatarajiwa kujiunga na timu ya kocha Roberto Mancini kwa mkopo hadi mwisho wa msimu, dili ambalo litaigharimu klabu hiyo ya Italia Pauni Milioni 1.5.
    Lukas Podolski arrives in Milan where he is set to join Inter on loan until the end of the season
    Lukas Podolski akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kuwasili Milan 
    Podolski holds up blue and black scarf as fans ask him questions and take pictures
    Podolski akiwa ameinua skafu ya Inter huku mashabiki wakimfurahia

    "Nimezungumza na Mancini na nafikiri ni kocha babu kubwa. Amenitaka na ninafurahi kuwa hapa. Naifahamu Serie A, ni ligi yenye ushindani sana. Nataka kuisaidia timu irudi kwenye Ligi ya Mabingwa (Ulaya). Nina ujumbe kwa mashabiki? Nina furaha, Forza Inter na tunatumai kuwa na msimu mzuri," amesema akizungumza Waandishi wa Habari jana.
    Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani ambaye ameshindwa kung'ara Arsenal, amebakiza mwaka mmoja na klabu hiyo ya London na huenda asirejee Emirates mwishoni mwa msimu iwapo mambo yatamuendea vizuri MIlan. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LUKAS PODOLSKI ATUA MILAN NA KUAHIDI MAKUBWA, MASHABIKI WAPAGAWA NAYE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top