• HABARI MPYA

  Jumamosi, Septemba 12, 2020

  ARSENAL YAANZA VYEMA LIGI ENGLAND, YAICHAPA 3-0 FULHAM

  ARSENAL imeanza vyema msimu mpya wa Ligi Kuu ya England baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Fulham waliorejea msimu huu, mabao ya Alexandre Lacazette dakika ya 18, mchezaji mpya Gabriel Magalhaes dakika ya 49 na Nahodha Pierre-Emerick Aubameyang dakika ya 57 Uwanja wa Craven Cottage Jijini London.
  Huo ni mwendelezo mzuri wa matokeo ya timu chini ya kocha Mikel Arteta msimu mpya, wakitoka kutwaa Ngao ya Jamii kwa ushindi wa penalti 5-4 kufuatyia sare ya 1-1 na mabingwa watetezi, Liverpool Agosti 29 Uwanja wa Wembley Jijini London.

  Nahodha Pierre-Emerick Aubameyang akishangilia baada ya kuifungia Arsenal bao la tatu leo Uwanja wa Craven Cottage Jijini London 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ARSENAL YAANZA VYEMA LIGI ENGLAND, YAICHAPA 3-0 FULHAM Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top