• HABARI MPYA

  Jumapili, Septemba 13, 2020

  SAMATTA ATOKEA BENCHI KIPINDI CHA PILI ASTON VILLA YAICHAPA MAN UNITED 1-0 VILLA PARK

  Na Mwandishi Wetu, BIRMINGHAM
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta jana ametokea benchi kipindi cha pili na kuisaidia klabu yake, Aston Villa kupata ushindi wa 1-0 dhidi ya Manchester United katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Villa Park Jijini Birmingham.
  Samatta aliingia dakika ya 66 kuchukua nafasi ya mfungaji wa bao pekee, Ollie Watkins ambaye alifunga dakika ya 16 akimalizia pasi ya kiungo Mmisri, Mahmoud Ahmed Ibrahim Hassan, maarufu kama Trezeguet.
  Timu hizo zilikubaliana kucheza mechi ya kirafiki wikiendi hii kwa sababu mechi zao za ufunguzi za Ligi Kuu ya England zimeahirishwa. 
  Man United ilikuwa waanze na Burnley Uwanja wa Turf Moor na Aston Villa walitakiwa kuwafuata Manchester City Uwanja wa Etihad.
  Na sababu ya kuahirishwa kwa mechi hizo ni kuzipa muda zaidi wa maandalizi Manchester City na Manchester United ambazo zilishiriki michuano ya klabu barani Ulaya hadi hatua za mwishoni.
  Kikosi cha Aston Villa kilikuwa: Steer; Cash/Ahmed El Mohamady dk72, Konsa, Mings, Targett; Hourihane, Luiz, McGinn, Trezeguet/Jota Peleteiro dk77, Watkins/Samatta dk66 na Grealish.
  Manchester United; Henderson; Dalot/ Williams dk70, Fosu-Mensah, Maguire, Shaw; McTominay/Galbraith dk46, van de Beek; Lingard, Rashford, James na Ighalo/Mengi dk60.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SAMATTA ATOKEA BENCHI KIPINDI CHA PILI ASTON VILLA YAICHAPA MAN UNITED 1-0 VILLA PARK Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top