• HABARI MPYA

  Jumamosi, Septemba 05, 2020

  WAZIRI KIGWANGALLA ASHANGAA MO DEWJI KUMTEUA MSAIDIZI WAKE BINAFSI KUWA CEO SIMBA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk HamisI Kigwangalla ametilia shaka uteuzi wa Msaidizi Binafasi wa Bilionea, Mohjamed ‘Mo’ Dewji, Barbara Gonzalez kuwa Mtendaji Mkuu mpya wa klabu ya Simba SC.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC, Mo Dewji leo amemtangaza Barbara Gonzalez kuwa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, akiziba nafasi ya Muafrika Kusini, Senzo Mazingisa Mbatha aliyehamia kwa watani, Yanga SC.
  Lakini saa chache baada ya uteuzi huo, Kigwangala akaandika kwenye ukurasa wake wa twitter; “Kuna ujanja na Kuna ujanja ujanja. Ujanja ni pale @SimbaSCTanzania tulipokubali kuhama kutoka kuwa Klabu ya Wanachama na kuwa Kampuni. Ujanja ujanja ni hiki kinachoendelea sasa hivi; hisa hazijalipiwa. PA wa mwekezaji ambaye hajalipia shares anateuliwa kuwa CEO,”.
  Kigwangalla ameongeza kwamba mabadiliko yaliyompa Mo Dewji Uenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC hayajakamilika kwa kuwa hajalipa Sh. Bilioni 20, lakini ajabu anafanya maamuzi anavyotaka.
  Mo Dewji akamjibu Kigwangalla katika mjadala uliovutia watu wengi wenye mawazo tofauti; “Mhe.Kigwangalla, sio utu kumuombea mtu yoyote apigwe mawe. Suala la uwekezaji Simba nililielezea kwenye interview na WasafiFM. Wengi wameelewa. Itafute. Kama bado hutaelewa, namba yangu unayo nipigie nitakufafanulia. Pia nisamehe kwamba mkopo wa pikipiki ulioniomba haikuwezekana,”.
  Hivi karibuni Mo Dewji alisema kwamba mfumo wa mabadiliko bado haujakamilika hivyo si wakati mwafaka kuzungumzia uwekezaji wake wa Sh. Bilioni 20 katika klabu hiyo. “Bilioni 20 zipo, kwa sasa kila mwaka natoa bilioni 3 kama ruzuku kwa klabu. Naamini asilimia kubwa ya Wanasimba wananielewa, kama hunielewi, basi,”alisema.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: WAZIRI KIGWANGALLA ASHANGAA MO DEWJI KUMTEUA MSAIDIZI WAKE BINAFSI KUWA CEO SIMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top