• HABARI MPYA

  Alhamisi, Septemba 03, 2020

  KAMPUNI YA STAR TIMES KUONYESHA LIVE LA LIGA MSIMU WA 2020/2021

  Na Asha Kigundula, DAR ES SALAAM
  KAMPUNI  ya StarTimes imetangaza kuanza kurusha moja kwa moja Michuano ya ligi kuu ya soka nchini Hispania (La Liga) kwa lugha ya Kifaransa kuanzia msimu huu wa 2020/21 kupita Chanel ya Sports Premium.
  StarTimes imekuja na Kampeni ya 'Soka Limenoga' ambapo pia wataendelea kuonyesha michuano ya Uefa National League, Uefa Europa League, FA Emirates Cup, Coppa Italia, Copa Del Rey na Ngao ya Jamii nchini Uiengereza kama kawaida.
  Meneja wa Masoko wa StarTimes, David Malisa amesema La Liga ndio ligi bora katika miaka 10 iliyopita mpaka sasa ndio maana imefanikiwa kutoka wachezaji bora wa dunia kwa muda huo wote hivyo wameamua kuwapa burudani wateja wao.

  "StarTimes tumekuja na kampeni  ya 'Soka Limenoga na msimu huu tutarusha ligi kuu ya soka nchini Hispania ambayo ndio ligi bora kwa sasa duniani katika miaka 10 mfululizo," alisema Malisa.
  Kwa upande wake mchambuzi wa Soka, Shaffih Dauda alisema ligi ya Hispania inacheza soka maridadi lenye matumizi mazuri ya akili kuliko nguvu (Sex football) naamini Watanzania watashuhudia ligi bora dunia.
  Jana saa 3 usiku StarTimes itarusha mchezo mkali wa Uefa National League kati ya Ujerumani dhidi ya Hispania kupitia World Football kwa malipo ya shilingi 20,000 kwa Antena na shilingi 21,000 kwa wenye Dish

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KAMPUNI YA STAR TIMES KUONYESHA LIVE LA LIGA MSIMU WA 2020/2021 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top