• HABARI MPYA

  Jumatatu, Septemba 28, 2020

  NI MIAMI HEAT NA LOS ANGELES LAKERS FAINALI NBA 2020

  KATIKA Ligi ya mpira wa Kikapu Marekani, Miami Heat wametawazwa kuwa mabingwa wa Eastern Conference baada ya kuifunga Boston Celtics 125-113.

  Pongezi kwa Bam Adebayo aliyefunga pointi 32 na rebounds 14 na Jimmy Butler pointi 22 kuiwezesha Miami Heat kushinda kwa series 4-2 na kutwaa taji hilo kwa mara ya sita – na sasa watakutana na Los Angeles Lakers ya akina LeBron James, mabingwa wa West kuwania taji la NBA 2020.

  Los Angeles Lakers jana iliichapa Denver Nuggets 117-107 na kutwaa ubngwa wa Western Conference.


  Miami Heat wametawazwa kuwa mabingwa wa Eastern Conference baada ya kuifunga Boston Celtics 125-113 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NI MIAMI HEAT NA LOS ANGELES LAKERS FAINALI NBA 2020 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top