• HABARI MPYA

  Jumatano, Septemba 09, 2020

  ADI YUSSUF APELEKWA TENA KWA MKOPO UINGEREZA, SAFARI HII AHAMISHIWA WREXHAM YA WALES

  Na Mwandishi Wetu, WREXHAM
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Abdillahie ‘Adi’ Yussuf amejiunga na Wrexham ya Wales inayocheza Ligi Daraja la Tano England, maarufu kama National League kwa mkopo wa hadi mwisho wa msimu kutoka Blackpool FC ya Daraja la Tatu.
  Wrexham inakuwa timu ya tatu Adi Yussuf kupelekwa kwa mkopo tangu asajiliwe Blackpool FC Mei mwaka jana kwa mkataba wa miaka miwili – baada ya awali kupelewa klabu yake ya zamani, Solihull Moors na Boreham Wood msimu uliopita.
  Yussuf alikuwemo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kilichoshiriki Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) Juni mwaka jana nchini Misri.

  Adi Yussuf amejiunga na Wrexham ya Daraja la Tano kwa mkopo kutoka Blackpool FC zote za England

  Alitua Blackpool baada ya kufunga mabao 21 katika mashindano yote Solihull Moors, yakiwemo mawili dhidi ya Seasiders kwenye mchezo wa marudiano wa Raundi ya Pili ya Kombe la FA na kuiwezesha timu hiyo kumaliza nafasi ya pili kwenye National League.
  Mchezaji huyo wa zamani wa akademi ya Leicester City, rekodi yake nzuri zaidi ya msimu ni kufunga mabao 29 katika mechi 39 akiwa na Oxford City msimu wa 2014- 2015 baada ya awali kuchezea Burton Albion, Mansfield Town na Crawley Town.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ADI YUSSUF APELEKWA TENA KWA MKOPO UINGEREZA, SAFARI HII AHAMISHIWA WREXHAM YA WALES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top