• HABARI MPYA

    Monday, September 07, 2020

    KROSI YA PRINCE DUBE, CHIRWA APIGA BAO PEKEE CHAMAZI AZAM FC YAICHAPA POLISI TANZANIA 1-0

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    BAO pekee la mshambuliaji Mzambia, Obrey Chirwa limetosha kuipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo wa mwisho wa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku wa leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
    Chirwa alifunga bao hilo dakika ya 45 kwa kichwa akimalizia krosi nzuri ya mshambuliaji mpya, Mzimbabwe Prince Dube kutoka upande wa kushoto wa Uwanja.
    Mechi nyingine za leo, KMC iliibuka na ushindi wa 4-0 dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, mabao ya Israel Mwenda, Hassan Kabunda, Abdul Hillary na Paul Peter.



    Nayo JKT Tanzania ikapata ushindi wa ugenini wa 1-0 dhidi ya wenyej, Kagera Sugar – bao pekee la Adam Adam dakika ya 16 Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KROSI YA PRINCE DUBE, CHIRWA APIGA BAO PEKEE CHAMAZI AZAM FC YAICHAPA POLISI TANZANIA 1-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top