• HABARI MPYA

  Jumatano, Septemba 16, 2020

  NUGGETS YAICHAPA LA CLIPPERS 104-98, YATINGA FAINALI WEST

  NYOTA Jamal Murray na Nikola Jokic Alfajiri ya leo wameiongoza Denver Nuggets kutinga Fainali ya Western Conference  kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2009 baada ya kuichapa Los Angeles Clippers 104-89 kwenye Game Ligi ya mpira wa kikapu Marekani na sasa watakutana na Los Angeles Lakers.

  Murray amefunga pointi 40, Jokic akapiga triple-double quarter ya tatu na kwa mara nyingine Denver ikiweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza ya NBA kihistoria kutoka nyuma kwa series 3-1 na kushinda mara mbili katika msimu mmoja.

  Kwa ujumla, kihistoria The Nuggets inakuwa timu ya tatu Marekani kwenye michezo mikubwa kutoka nyuma kwa 3-1 mara mbili katika playoffs moja na kushinda, ikiungana na Kansas City Royals 1985 na Minnesota Wild mwaka 2003.

  Nikola Jokic na Jamal Murray wa Denver Nuggets wakipongezana kwa ushindi dhidi ya LA Clippers PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Nayo Miami Heat imeifunga Boston Celtics 117-114 katika Game 1ya fainali ya Eastern Conference – kwa mchango mkubwa wa Jimmy Butler na Bam Adebayo.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NUGGETS YAICHAPA LA CLIPPERS 104-98, YATINGA FAINALI WEST Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top