• HABARI MPYA

    Friday, September 25, 2020

    BAYERN MUNICH WAIGONGA SEVILLA 2-1 NA KUTWAA UEFA SUPER CUP


    Wachezaji wa Bayern Munich wakishangilia na taji la UEFA Super Cup baada ya ushindi wa 2-1 dhid- ya Sevilla usiku wa jana Uwanja wa Puskas Arena Jijini Budapest, Hungary. 

    Sevilla ilitangulia kwa bao la Lucas Ocampos dakika ya 13 kwa penalti baada ya Ivan Rakitic kuangushwa kwenye boksi, lakini Leon Goretzka akaisawazishia Bayern Munich dakika ya 34, kabla ya bao la Robert Lewandowski kukataliwa na mchezo ukaisha 1-1 ndani ya dakika 90.

    Katika dakika 30 za nyongeza ndipo mtokea benchi, Javi Martinez akaifungia bao la ushindi Bayern Munich dakika ya 104, mabingwa wa Ligi ya Mabingwa wakiwaangusha mabingwa wa Europa League mbele ya mashabiki 20,000 kwenye Uwanja unaochukua watazamaji 67,000, kati yao 500 wakisafiri kutoka Hispania na 1,000 kutoka Ujerumani 

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BAYERN MUNICH WAIGONGA SEVILLA 2-1 NA KUTWAA UEFA SUPER CUP Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top