• HABARI MPYA

  Sunday, September 20, 2020

  AZAM FC YAREJEA KILELENI LIGI KUU BAADA YA KUICHAPA MBEYA CITY 1-0 UWANJA WA SOKOINE

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM

  TIMU ya Azam FC imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania ya Bara jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. 

  Pongezi kwa mafungaji wa bao hilo pekee, kiungo wa kimataifa wa Rwanda, Ally Niyonzima dakika ya 25 akimalizia kona ya kiungo Mzimbabwe, Never Tigere.

  Na kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi tisa baada ya kucheza mechi tatu, ikishinda 1-0 zote na kurejea kilieleni mwa Ligi Kuu.

  Kiungo wa kimataifa wa Rwanda, Ally Niyonzima ameifungia Azam FC bao pekee ikiilaza Mbeya City 1-0 leo 


  Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, Coastal Union imelazimishwa sare ya bila kufungana na Dodoma Jiji FC Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga. 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAREJEA KILELENI LIGI KUU BAADA YA KUICHAPA MBEYA CITY 1-0 UWANJA WA SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top