• HABARI MPYA

  Jumatatu, Septemba 07, 2020

  KAPTENI RAMOS APIGA MBILI HISPANIA YAICHAPA UKRAINE 4-0

  Beki na Nahodha, Sergio Ramos akishangilia baada ya kuifungia Hispania mabao mawili dakika ya tatu kwa penalti na 29 katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Ukraine kwenye mchezo wa Kundi la Nne Ligi ya Mataifa ya Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Alfredo Di Stefano Jijini Madrid. Mabao mengine ya Hispania yalifungwa na Ansu Fati dakika ya 32 na Ferran Torres dakika ya 84. Mechi nyingine ya kundi hilo jana, Uswisi ililazimishwa sare ya 1-1 na Ujerumani Uwanja wa St. Jakob-Park Jijini Basel, Ilkay Gundogan akianza kuwafungia Ujerumani dakika ya 14, kabla ya Silvan Widmer kuwasawazishia wenyeji dakika ya 57 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KAPTENI RAMOS APIGA MBILI HISPANIA YAICHAPA UKRAINE 4-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top