• HABARI MPYA

  Jumatano, Septemba 16, 2020

  SAMATTA ABAKI BENCHI HADI MWISHO ASTON VILLA YAWACHAPA BURTON ALBION 3-1 CARABAO

  Na Mwandishi Wetu, STAFFORDSHIRE

  MSHAMBULAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku wa jana alibaki benchi kwa muda wote, klabu yake, Aston Villa ikiibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya wenyeji, Burton Albion kwenye mchezo wa Raundi ya pili ya Kombe la Ligi England, maarufu kama CarabaoCup Uwanja wa Pirelli huko Burton-upon-Trent, Staffordshire.

  Mabao ya Aston Villa jana yalifungwa na mshambuliaji mpya aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 33 kutoka Brentford ya Daraja la Kwanza Ollie Watkins dakika ya 39, kuingo na Nahodha Jack Grealish dakika ya88 na mshambulaji Keinan Davis dakika ya 90, wakati bao pekee la Burton lilifungwa na beki Colin Daniel dakika ya 64.

  Kwenye mchezo uIiopita wa kirafiki Aston Villa ikishinda 1-0 dhidi ya Manchester United Uwanja wa Villa Park Jijini Birmingham, Samatta aliingia Samatta alitokea benchi dakika ya 66 kuchukua nafasi ya mfungaji wa bao hilo pekee, Ollie Watkins.

  Mbwana Samatta hakutumika jana klabu yake, Aston Villa ikiibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Burton Albion

  Na bila shaka jana kocha Dean Smith aliamua kumpumzisha Samatta kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya England dhid ya Sheffield United Jumatatu Saa 2:00 usiku Uwanja wa Villa Park. 

  Kikosi cha Burton Albion kilikuwa: Sharman-Lowe, Fox, Brayford/Gallacher dk25, Bostwick, Wallace, Quinn, Edwards/Powell dk66, Akins, Lawless/Gilligan dk66, Daniel na Hemmings.

  Aston Villa: Nyland, Elmohamady, Hause, Mings, Taylor, J. Ramsey/Douglas Luiz dk71, Nakamba, Lansbury, El Ghazi/Jota dk80, Watkins/Davis dk71 na Grealish.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SAMATTA ABAKI BENCHI HADI MWISHO ASTON VILLA YAWACHAPA BURTON ALBION 3-1 CARABAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top