• HABARI MPYA

  Jumapili, Septemba 13, 2020

  MESSI ATOKEA BENCHI BARCELONA YASHINDA 3-1 MECHI YA KIRAFIKI

  NYOTA Muargentina, Lionel Messi jana amecheza mechi yake ya kwanza Barcelona tangu jaribio lake la kuondoka lizimwe.
  Messi mwenye umri wa miaka 33 aliingia dakika ya 46 kuchukua nafasi ya mshambulaji Mdenmark Martin Braithwaite, Barcelona ikiibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Gimnastic de Tarragona katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Johan Cruyff mjini Sant Joan Despí.
  Mabao ya Barcelona ambayo sasa ipo chini ya kocha Mholanzi, Ronald Koeman yalifungwa na Ousmane Dembele dakika ya tano, Antoine Griezmann dakika ya 17 kwa penalti na Phillipe Coutinho dakika ya 51  kwa penalti pia, wakati bao pekee la Gimnastic de Tarragona lilifungwa na Javier Bonilla dakika ya 30.

  Lionel Messi jana amecheza kwa dakika ya 45 Barcelona ikiibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Gimnastic Tarragona 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MESSI ATOKEA BENCHI BARCELONA YASHINDA 3-1 MECHI YA KIRAFIKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top