• HABARI MPYA

  Jumamosi, Septemba 26, 2020

  FERNANDES AFUNGA LA USHINDI MAN UNITED YAICHAPA BRIGHTON 3-2

  TIMU ya Manchester United imepata ushindi wa kwanza katika Ligi Kuu ya England baada ya kuichapa  Brighton & Hove Albion 3-2 jioni ya leo Uwanja wa The Amex.

  Pogezi kwa mfungaji wa bao la ushindi, kiungo Mreno Bruno Fernandes dakika ya tisa ya muda wa nyongeza baada ya kutimia dakika 90 ambaye alifunga kwa penalti iliyotolewa kwa msaada ya marudio ya picha za video (VAR) kufuatia Neal Maupay kuunawa mpira.

  Na bao hilo lilipatikana baada ya wenyeji, Brighton kusawazisha dakika tano zilizotangulia kupitia kwa Solly March na mchezo kuwa 2-2.


  Wachezaji wa Manchester United wakimpongeza Bruno Fernandes baada ya kufunga bao la ushindi wakiichapa  Brighton & Hove Albion 3-2 jioni ya leo Uwanja wa The Amex
   

  Ni Maupay alianza kuifungia Brighton & Hove Albion kwa penalti dakika ya 40, kabla ya Lewis Dunk kujifunga dakika ya 43 kuisawazishia Manchester United na Marcus Rashford kufunga la pili dakika ya 55.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: FERNANDES AFUNGA LA USHINDI MAN UNITED YAICHAPA BRIGHTON 3-2 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top