• HABARI MPYA

  Jumanne, Septemba 08, 2020

  MBAPPE ANA COVID 19, KUKOSEKANA LEO UFARANSA NA CROATIA

  MSHAMBULIAJI wa Paris Saint-Germain, Kylian Mbappe jana alipimwa na kukutwa na ugonjwa wa COVID-19 na atakosekana kwenye kikosi cha Ufaransa leo kikimenyana na Croatia katika mchezo wa Kundi la Tatu Ligi ya Mataifa Ulaya Uwanja wa Stade de France Jijini Paris.
  Mbappe aliyefunga bao pekee kwenye ushindi wa 1-0 dhidi ya Sweden 1-0 Jumamosi, hilo likiwa bao lake la 14 kwenye timu yake ya taifa – alirudishwa nyumbani jana.
  Shirikisho limesema Mbappe alifuzu vipimo vya awali kabla ya kuungana na wachezaji wenzake mazoezini na akafuzu pia vipimo vya pili Jumatano iliyopita kuelekea mechi na Sweden. 

  Kylian Mbappe atakosekana leo Ufaransa ikimenyana Croatia Ligi ya Mataifa Ulaya Uwanja wa Stade de France Jijini Paris PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MBAPPE ANA COVID 19, KUKOSEKANA LEO UFARANSA NA CROATIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top