• HABARI MPYA

  Jumatatu, Septemba 21, 2020

  LUSAJO APIGA MBILI KMC YAREJEA KILELENI LIGI KUU BAADA YA KUICHAPA 2-1 MWADUI FC SHINYANGA

  Na Mwandishi Wetu, SHNYANGA

  TIMU ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni (KMC) imefanikiwa kurejea kileleni mwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Mwadui FC mchana wa leo Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga.

  Kwa ushindi huo, KMC inayofundishwa na Habib Kondo inafikisha pointi tisa, sawa na Azam FC ambayo kwa kuzidiwa wastani wa mabao, inaangukia nafasi ya pili.

  Na haukuwa ushindi mwepesi kwa KMC leo, kwani ililazimika kutoka nyuma kwa mabao ya mshambuliaji wake mpya, Relliant Lusajo dakika ya 77 na 84, baada ya Issa Shaaban kutangulia kuifungIa Mwadui FC dakika ya 11.


  Mshambuliaji mpya, Relliant Lusajo akishangila baada ya kuifungia KMC mabao mawilI leo katika ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Mwadui FC mkoani Shinyanga

  Mchezo mwingine wa Ligi Kuu leo, Ruvu Shooting imepata ushindi wa kwanza wa msimu baada ya kuilaza Gwambina FC 1-0 Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani – bao pekee la Fully Zullu Maganga dakika ya 41.

  Na baada ya kutoa sare ya 0-0 na Mtibwa Sugar mkoani Morogoro na kufungwa 1-0 na Ihefu SC Jijini Mbeya, sasa Ruvu Shooting inayofundishwa na Charles Boniface Mkwasa inafikisha pointi nne.  

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LUSAJO APIGA MBILI KMC YAREJEA KILELENI LIGI KUU BAADA YA KUICHAPA 2-1 MWADUI FC SHINYANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top