• HABARI MPYA

  Jumapili, Septemba 06, 2020

  NAMUNGO FC NA BIASHARA UNITED ZAUANZA VYEMA MSIMU MPYA WA LIGI KUU TANZANIA BARA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU za Namungo FC ya Lindi na Biashara United ya Mara zimeuanza vyema msimu mpya wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa 1-0 zote dhidi ya Coastal Union ya Tanga na Gwambina FC ya Mwanza.
  Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi bao pekee la Bigirimana Blaise dakika ya 64 lilitosha kuwapa wenyeji, Namungo FC ushindi wa 1-0.
  Na Uwanja wa Karume, Musoma mkoani Mara – bao pekee Kelvin Friday dakika ya 88 likawapa ushindi wa 1-0 Biashara United.


  Mechi nyingine tatu zinaendelea jioni hii, mabingwa watetezi, Simba wakimenyana na Ihefu SC iliyopanda Ligi Kuu msimu huu Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya, Mtibwa Sugar na Ruvu Shooting Uwanja wa CCM Gairo mkoani Morogoro.
  Saa 1:00 usiku wa leo mechi zitahitimishwa kwa mtanange kati ya vigogo, Yanga SC na Tanzania Prisons ya Mbeya Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Mbeya.
  Mechi za kwanza za Ligi Kuu zitakamilishwa kesho kwa KMC kuwaalika Mbeya City Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, Kagera Sugar kuwa wenyeji wa JKT Tanzania Uwanja wa Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera na Azam FC kuwakaribisha Polisi Tanzania Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NAMUNGO FC NA BIASHARA UNITED ZAUANZA VYEMA MSIMU MPYA WA LIGI KUU TANZANIA BARA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top