• HABARI MPYA

  Jumatano, Agosti 05, 2020

  PAMBANO LA MWAKINYO NA MKONGO KUWA LIVE AZAM TV

  Na mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  PAMBANO la ndondi baina ya Hassan Mwakinyo na Tshibangu Kayembe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kuwania taji la WBF Intercontinental uzito wa Super Welter litakalofanyika Agosti 14, mwaka huu ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam litaonyeshwa moja kwa moja na AzamSports2.
  Hilo litakuwa pambano la kwanza la Mwakinyo mwaka huu na kwa ujumla la kwanza tangu amshinde kwa pointi Arnel Tinampay wa Ufilipino Novemba 29, mwaka jana Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
  Katika mapambano 18 ya awali ya Mwakinyo anayejulikana kwa jina la utani Champez mwenye umri wa miaka 25, ameshinda 16, kati ya hayo 11 kwa Knockout (KO) na kupoteza mawili, yote kwa KO.
  Pambano lake lililopita, Kayembe alimpiga Mtanzania Cossmas Cheka kwa KO ukumb wa Grand Hotel de Kinshasa Jijini Kinshasa Agosti 25 mwaka juzi na kutwaa taj la UBO International uzito wa Super Light.
  Kwa ujumla Kayembe mwenye umri wa miaka 24, amepigana mapambano 12, ameshinda tisa, matatu kwa KO na ametoa droo matatu. 
  Kutakuwa na mapambano ya utangulizi pia siku hiyo; Tonny Rashid Vs Tinashe Mzidwana, Haidary Mchanjo  Vs Baina Mazola, Issa Nampepeche Vs Kharid Manjee, Suleiman Kidunda Vs Shaaban Kaoneka, Juma Choki Vs Emmanuel Mwakyembe na Ismail Galiatano Vs Saidi Zungu. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: PAMBANO LA MWAKINYO NA MKONGO KUWA LIVE AZAM TV Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top