• HABARI MPYA

  Jumatano, Agosti 05, 2020

  YANGA SC YAVUNJA NA BENCHI LAKE LOTE LA UFUNDI BAADA YA KUFUKUZA NUSU YA WACHEZAJI WAKE

  Na mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  IKITOKA kuachana na takriban nusu ya wachezaji iliyokuwa nao msimu uliopita, klabu ya Yanga SC pia imevunja pia benchi lake la Ufundi.
  Kocha Msaidizi, Charles Boniface Mkwasa, Kocha wa makipa, Manyika Peter, Meneja Abeid Mziba, Mtunza Vifaa, Freddy Mbuna na Mchua Misuli, Jacob Onyango wanaungana na aliyekuwa Kocha Mkuu, Mbelgiji Luc Eymael.
  Wengine waliokumbwa na ‘paranja’ hilo ni Kocha wa mazoezi ya viungo, Riedoh Berdien, Mchua Misuli, Fareed Cassim wote kutoka Afrka Kusini na Daktari Shecky Mngazija.
  Hatua hiyo ilifuatia Yanga SC kuachana na wachezaji 14, saba baada ya kumaliza mikataba na wengine saba wakisitishiwa mikataba yao kwa sababu mbalimbali ikiwemo nidhamu na viwango vyao kutokidhi mahitaji ya klabu.
  Waliomaliza mikataba ni mabeki Jaffary Mohamed, Andrew Vincent ‘Dante’, viungo Mohamed Issa ‘Banka’ na Mrisho Ngassa wote wazawa, aliyekuwa Nahodha, kiungo Papy Kabamba Tshishimbi, washambuliaji David Molinga ‘Falcao’ wote kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Tariq Seif, mzawa pia.
  Waliositishiwa mikataba ni mabeki Ally Mtoni ‘Sonso’, Muharami Issa ‘Marcelo’, Ali Ali, viungo Patrick Sibomana (Rwanda), Erick Kabamba (Zambia), Rapahael Daudi na mshambuliaji Yikpe Gislain (Ivory Coast). 
  Baada ya kuachana na wachezaji hao 14, Yanga SC ipo kwenye mazungumzo na mabeki wake wakongwe wawili, Juma Abdul na Kelvin Yondan waliomaliza mikataba.
  Wachezaji 15 tu kutoka kikosi cha msimu uliopita wamepitishwa kubaki ambao ni makipa Mkenya Farouk Shikhalo, Metacha Mnata na Ramadhan Kabwili na mabeki Paul Godfrey ‘Boxer’ na Mghana, Lamine Moro.
  Wengne ni viungo Mnyarwanda Haruna Niyonzima, Mghana Bernard Morrison, Feisal Salum, Juma Mahadhi, Adeyoum Ahmed, Said Juma ‘Makapu’, Balama Mapinduzi, Deus Kaseke, Ditram Nchimbi na Abdulaziz Makame.
  Tayari Yanga SC imesajili wachezaji wanne wapya, ambao ni mabeki Yassin Mustapha kutoka Polisi Tanzana ya Kilimanjaro, Bakari Mwamnyeto kutoka Coastal Union ya Tanga, kiungo Zawadi Mauya kutoka Kagera Sugar na mshambuliaji Waziri Junior kutoka Mbao FC ya Mwanza iliyoshuka Daraja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA SC YAVUNJA NA BENCHI LAKE LOTE LA UFUNDI BAADA YA KUFUKUZA NUSU YA WACHEZAJI WAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top