• HABARI MPYA

  Alhamisi, Agosti 06, 2020

  MAN UNITED YATINGA ROBO FAINALI UEFA EUROPA LEAGUE

  Mshambuliaji Anthony Martial akishangilia baada ya kuifungia Manchester United bao la ushindi dakika ya 88 ikiwalaza LASK ya Austria 2-1 katika mchezo wa marudiano Hatua ya 16 Bora UEFA Europa League usiku wa jana Uwanja wa Old Trafford. LASK walitangulia kwa bao la Philipp Wiesinger dakika ya 55 kabla ya Jesse Lingard kuisawazishia Man United dakika mbili baadaye na sasa kikosi cha Ole Gunnar Solskjaer kinatinga Robo fainali ya Europa League kwa ushindi wa jumla wa 7-1 baada ya kushinda 5-0 kwenye mchezo wa kwanza ugenini 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAN UNITED YATINGA ROBO FAINALI UEFA EUROPA LEAGUE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top