• HABARI MPYA

    Thursday, August 06, 2020

    AZAM FC YAMSAJILI DAVID KISSU, KIPA MTANZANIA ALIYEKUWA ANACHEZA SOKA YA KULIPWA NCHINI KENYA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KLABU ya Azam FC imekamilidha usajili wa kipa wa kimataifa wa Tanzania, David Mapigano Kissu aliyesaini mkataba wa miaka miwili kutoka Gor Mahia ya Kenya.
    Kissu ambaye yumo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, usajili wake ni sehemu ya mapendekezo ya benchi la ufundi la Azam FC.
    Kipa huyo aliyechezea timu za Njombe Mji na Singida United, kabla ya kutimkia nchini Kenya, amekuwa na msimu nzuri akiwa na Gor Mahia, takwimu zikionyesha amecheza jumla ya mechi 15, huku akiwa hajaruhusu wavu wake kuguswa (clean sheet) katika mechi tisa kati ya hizo.
    Nyota huyo aliyekuwa kipa namba moja wa Gor Mahia, pia aliweka rekodi ya kufunga bao, akifunga kwa mpira mrefu wa moja kwa moja, wakati Gor Mahia ikiilaza Bandari mabao 3-0.
    Huo ni usajili wa tano kwenye kikosi cha Azam FC kwa ajili ya msimu ujao, wengine waliosajiliwa wakiwa ni viungo watupu Awesu Awesu kutoka Kagera Sugar ya Bukoba, Ayoub Lyanga kutoka Coastal Unon ya Tanga, Ismail Aziz Kada kutoka Tanzania Prisons ya Mbeya na Ally Niyonzima kutoka Rayon Sport ya kwao, Rwanda.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC YAMSAJILI DAVID KISSU, KIPA MTANZANIA ALIYEKUWA ANACHEZA SOKA YA KULIPWA NCHINI KENYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top