• HABARI MPYA

  Jumatano, Januari 23, 2019

  SIMBA SC YAINGIA NUSU FAINALI KOMBE LA SPORTPESA, KUMENYANA NA BANDARI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SIMBA SC imefanikiwa kuingia Nusu Fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya AFC Leopards ya Kenya jioni ya leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam. 
  Ushindi huo unakuja siku nne baada ya Simba SC kufungwa 5-0 na wenyeji wao, AS Vita mjini Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika mchezo wa Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika.
  Kwa ushindi huo, Simba SC inayofundishwa na kocha Mbelgiji Patrick Aussems, itakutana na Bandari ya Mombasa nchini Kenya pia katika Nusu Fainali, wakati FC iliyowatoa mabingwa watetezi, Gor Mahia watamenyana na Kariobangi Sharks iliyowatoa Yanga SC. 
  Mshambuliaji Mganda, Emmanuel Arnold Okwi aliifungia Simba SC bao la kwanza dakika ya 13 kwa shuti akimalizia krosi ya beki kutoka Brukina Faso, Zana Coulibally.
  Wachezaji wa Simba SC wakishangilia bao lao la kwanza leo Uwanja wa Taifa  

  Mfungaji wa bao la pili la Simba SC, Clatous Chama akimtoka mchezaji wa AFC Leopards

  Emmanuel Okwi akimtoka mchezaji wa AFC Leopards ya Kenya

  Mshambuliaji wa Simba SC, Meddie Kagere akimtoka mchezaji wa AFC Leopards 

  Mashabiki wa Simba SC wakifurahi leo Uwanja wa Taifa siku chache baada ya kufungwa 5-0 na AS Vita mjini Kinshasa  

  Okwi akamsetia kiungo Mzambia, Clatous Chama kuifungia Simba SC bao la pili dakika ya 48 kabla ya Vincent Oburu kuidungia AFC Leopards, zamani Abaluhya bao la kufutia machozi dakika ya 61.
  Kikosi cha Simba SC kilikuwa: Aishi Manula, Rashid Juma, Zana  Coulibally, Lamine Moro, Pascal Wawa/Juuko Murshid dk46, Jonas Mkude/James Kotei dk46, Hassan Dilunga/Mohammed ‘Mo’ Ibrahim dk76, Haruna Niyonzima, Hunlede Kissimbo/Meddie Kagere dk46, Emmanuel Okwi/Muzamil Yassin dk66 na Clatous Chama
  Afc leopards: Adira Jairus, Kipyegon Isaac/Mburu Moses dakika ya 85, Oduro Isaac, Kamura Robinson, Seda Edward, Marita Brian, Whyvonne Isuza, Mukangula Eugene/Ochuka Clark dk79, Wayyeka Tutawe/Vincent Oburu dk50, Okaka Aziz/Marita Brian na Odenyi Jaffar/Sikhayi Dennis dk75.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAINGIA NUSU FAINALI KOMBE LA SPORTPESA, KUMENYANA NA BANDARI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top