• HABARI MPYA

  Thursday, January 31, 2019

  TAIFA STARS KUMENYANA NA SUDAN KUWANIA TIKETI YA CHAN YA 2020 ETHIOPIA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TANZANIA itaanza na Sudan katika mechi za kufuzu Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) zinazotarajiwa kufanyika mwakani nchini Ethiopia.
  Katika droo iliyopangwa jana makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) mjin Cairo, Misri kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati Kenya itamenyana na Burundi, Sudan Kusini na Uganda na Somalia dhidi ya Rwanda.
  Tanzania imeshiriki fainali moja tu za CHAN mwaka 2009 nchini Ivory Coast tena baada ya kuitoa Sudan katika hatua ya mwisho ya mchujo.

  Ibrahim Ajibu mmoja wa nyota wanaotarajiwa kuunda kikosi cha Tanzania cha CHAN

  Baada ya kumaliza nafasi tatu katika Kundi A mwaka 2009 mjini Abidjan nyuma ya Zambia na Senegal zilizokwenda Nusu Fainali, Tanzania imeshindwa kurudia mafanikio hayo kwenye michuano hiyo.
  Ikiwa chini ya kocha Mnigeria, Emmanuel Amunike kwa sasa, Taifa Stars itakuwa na wakati mgumu mbele ya Sudan ambayo ni moja ya timu zinazopewa nafasi ya kufuzu AFCON ya Ethiopia 2020.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TAIFA STARS KUMENYANA NA SUDAN KUWANIA TIKETI YA CHAN YA 2020 ETHIOPIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top