• HABARI MPYA

  Jumamosi, Januari 26, 2019

  KMC YATINGA 16 BORA KOMBE LA TFF, MBEYA CITY YAWATOA WABABE WA SIMBA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni (KMC) imefanikiwa kuingia hatua ya 16 Bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Pan Africans Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.
  Ushindi huo umetokana na mabao ya Elias Maguri dakika ya 27, Chrles Ilamfya dakika ya 62, Mohammed Rashid dakika ya 67, Abdil Hillary dakika ya 70 na Salum Chukwu dakika ya 90 na ushei, wakati bao pekee la mabingwa wa zamani wa Tanzania, Pan limefungwa na Abdul Masikini dakika ya 90.
  Kwa ushindi huo, KMC iliyopanda Ligi Kuu msimu huu itakutana na mshindi kati ya Mtibwa Sugar na Maji Maji FC ya Songea. 

  Nayo Kagera Sugar imeitupa nje Mbeya Kwanza kwa penalti 4-3 kufuatia sare ya 2-2 katika mchezo mwingine wa hatua ya 32 Bora uliofanyika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.  
  Na safari ya Mashujaa FC waliowatoa mabingwa wa Tanzania, Simba SC katika hatua ya 64 Bora  imefupishwa na Mbeya City leo baada ya kuchapwa 1-0 mjini Kigoma,
  Lipuli FC ya Iringa ikaitoa Polisi Tanzania kwa penalti 3-2 baada ya sare ya 1-1 Uwanja wa Ushirika mjini  Moshi, wakati Alliance FC imeifunga La Familia 2-0 Uwanja wa Nyamagana mjini Mwanza.
  Dodoma FC ya kocha Jamhuri Kihwelo imeitoa Transit Camp kwa penalti 5-4 kufuatia sare ya 1-1 Uwanja wa Jamhiri mjini Dodoma.
  Mechi za jana Coastal Union ya Tanga iliwachapa Kitayosce 2-0 huko Moshi mkoani Kilimajaro na kutinga hatua ya 16 Bora, African Lyon iliitupa nje Friends Rangers kwa penalti 4-2 kufuatia sare ya 0-0 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam na Dar City ikaitoa Cosmopolitan kwa penalti pia, 4-2 baada ya sare ya 0-0.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KMC YATINGA 16 BORA KOMBE LA TFF, MBEYA CITY YAWATOA WABABE WA SIMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top