• HABARI MPYA

  Friday, January 25, 2019

  MONACO YAMTIMUA THIERRY HENRY BAADA YA SIKU 104 KAZINI

  KLABU ya Monaco ya Ufaransa jana usiku imemfukuza kocha wake Thierry Henry licha ya kumuhakikishia kibarua chake kipo salama mapema wakati wanamuajiri siku 104 zilizopita.
  Monaco sasa ionataka kumridisha kocha wake wa zamani, Leonardo Jardim ambaye ndiye aliyendolelwa nafasi yake ikachukuliwa na Henry miezi mitatuntu iliyopita. 
  Wakala mkubwa na maarufu, Jorge Mendes ambaye amekuwa akifanya kazi na Monaco katika masuala ya usajili siku za karibuni, inaaminika ndiye aliyesuka mpango wa Jardim kurudi. 
  Thierry Henry amefukuzwa Monaco licha ya kuhakikishiwa kibarua chake kipo salama mapema wakati aanamuajiri 

  Henry, aliyesaini mkataba wa miaka mitatu mwesi Oktoba, amehakikishiwa kulipwa stahiki zake zote baada ya kufukuzwa.
  Inafahamika Makamu wa Rais wa klabu, Vadim Vasilyev alimuambia Henry atabakia Monaco licha ya matokeo mabaya klabu hiyo ikishinda mechi mbili tu kati ya 12 za Ligi. 
  Baada ya kipigo cha 5-1 cha Strasbourg mwishoni mwa wiki iliyopita, Monaco pia ilifungwa na timu ya Daraja la kwanza, Metz katika mechi ya Kombe la Ufaransa usiku wa Jumanne na. 
  Henry anaondoka baada ya kusajili wachezaji wake mwenyewe mwezi huu, ambao ni beki Naldo na Cesc Fabregas kutoka Chelsea. 
  Fabregas alicheza pamoja na Henry klabu ya Arsenal na inafahamika alivutiwa kujiunga na Monaco sababu ya mchezaji mwenzake huyo wa zamani, lakini sasa atafanya kazi na kocha mwingine. 
  Mspaniola huyo hakuonyeshwa dalili zozote katika mazungumzo ya kumsajili kama Henry yuko hatarini kufukuzwa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MONACO YAMTIMUA THIERRY HENRY BAADA YA SIKU 104 KAZINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top