• HABARI MPYA

  Jumatano, Januari 16, 2019

  SIMBA SC KUONDOKA KESHO BILA BOCCO KWENDA KINSHASA KUWAFUATA VITA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  NAHODHA wa Simba SC, John Raphael Bocco hatasafiri na timu kesho kwenda Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwa ajili ya mchezo wa Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, AS Vita Jumamosi. 
  Daktari wa Simba SC, Yassin Gembe amewaambia Waandishi wa Habari leo mjini Dar es Salaam kwamba Bocco anatakuwa kuwa nje kwa siku 10 baada ya kuumia kwenye Jumamosi iliyopita kwenye mchezo wa kwanza wa Kundi D dhidi ya Jeunesse Sportive de la Saoura, ijulikanayo kama JS Saoura ya Algeria.
  Katika mchezo huo ambao Simba SC ilishinda 3-0 dhidi ya JS Saoura au JSS Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam, mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Arnold Okwi akifunga bao moja na kuseti mawili mawili mbele ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa.

  John Bocco hatasafiri kesho kwenda Kinshasa kwa ajili ya mchezo dhidi ya AS Vita Jumamosi

  Bocco maarufu kwa jina la utani, Adebayor aliumia dakika ya 34 na kutolewa nje kwa machela kabla ya nafasi yake kuchukuliwa na mshambuliaji mwenzake, Meddie Ksgere kutoka Rwanda aliyekwenda kufunga mabao mawili kwenye ushindi huo. 
  Simba SC itacheza mechi yake ya pili ya Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika Jumamosi wiki hii mjini Kinshasa dhidi ya wenyeji, AS Vita ambao mechi yao ya kwanza walifungwa 2-0 na wenyeji, Al Ahly Uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria. JS Saoura watakuwa wenyeji wa Ahly siku hiyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA SC KUONDOKA KESHO BILA BOCCO KWENDA KINSHASA KUWAFUATA VITA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top