• HABARI MPYA

  Friday, January 25, 2019

  KOMBE LA SPORTPESA LAREJEA KENYA, MBAO NA SIMBA KUWANIA NAFASI YA TATU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Kariobangi Sharks imefanikiwa kuingia fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup baada ya ushindi wa penalti 6-5 kufuatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 dhidi ya Mbao FC ya Mwanza.
  Sasa kwa mara nyingine fainali ya SportPesa Super Cup nchini Tanzania itazikutanisha timu za Kenya baada ya wenyeji kuondolewa mapema kama ilivyokuwa mwaka 2017.
  Na hizo ni Kariobangi Sharks na Bandari FC ya Mombasa ambayo yenyewe imetinga fainali kwa kuwatoa vigogo wa Tanzania, Simba SC leo kwa kuwachapa mabao 2-1.

  Mwaka jana nchini Kenya, wenyeji Gor Mahia wakitwaa taji hilo kwa mara ya pili walikutana na Simba SC ya Tanzania na kuibuka na ushindi wa 2-1 katika fainali iliyopigwa Uwanja wa Afraha mjini Nakuru.
  Lakini Gor Mahia msimu huu walitupwa nje mapema tu na Mbao FC kwa mikwaju ya penalti baada ya sare ya 1-1 kwenye mechi za Robo Fainali.
  Gor Mahia pia ndiyo mabingwa wa kwanza wa michuano ya SportPesa Super Cup mwaka 2017 wakiwafunga mahasimu wao wa Kenya, AFC Leopards 3-0. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KOMBE LA SPORTPESA LAREJEA KENYA, MBAO NA SIMBA KUWANIA NAFASI YA TATU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top