• HABARI MPYA

  Wednesday, January 30, 2019

  MAN UTD YAICHOMOLEA BURNLEY DAKIKA YA MWISHO OLD TRAFFORD

  Victor Lindelof akiondoka kishujaa baada ya kuifungia Manchester United bao la kusawazisha dakika ya pili ya muda wa nyongeza baada ya kutimia dakika 90 wakitoa sare ya 2-2 na Burnley katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa jana Uwanja wa Old Trafford mjini Manchester. Mabao ya Ashley Barnes dakika ya 51 na Chris Wood dakika ya 81 yalikaribia kuipa ushindi wa ugenini Burnley, kabla ya Pogba kuifungia United la kwanza kwa penalti zikiwa zimesalia dakika tatu mchezo kwisha.
  Kwa kunusurika na kichapo, Man United wanafikisha pointi 45 baada ya kucheza mechi 24, wakiendelea kushika nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu, wakati Burnley inafikisha pointi 23 katika mechi ya 24 ikipanda hadi nafasi ya 15 kutoka ya 17 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UTD YAICHOMOLEA BURNLEY DAKIKA YA MWISHO OLD TRAFFORD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top