• HABARI MPYA

  Wednesday, January 23, 2019

  'SELFIE' YAMTIA LAWAMANI RONALDO HAKUJALI KUHUSU SALA

  GWIJI wa England, Gary Lineker amesikitishwa na kitendo cha Cristiano Ronaldo kuposti picha aliyojipiga ‘selfie’ akiwa kwenye ndege yake binafasi kipindi hiki ambacho mchezaji mpya wa Cardiff City, Emiliano Sala anahofiwa kufa kwenye ajali ya ndege.
  Ronaldo aliposti selfie yake katika siku ambayo Emiliano Sala alipata ajali akiwa kwenye ndege binafsi anatoka Ufaransa anakwenda Uingereza kuanza maisha mapya Cardiff.
  Sala aliposti picha sambamba na maelezo 'kwaheri ya mwisho' kwa wachezaji wenzake wa zamani, saa kadhaa kabla ya ndege maalum aliyokodiwa kuanguka maeneo ya England.
  Mshambuliaji huyo Muargentina alikamilisha uhamisho wake wa Pauni Milioni 15 kujiunga na Cardiff City Jumamosi kabla ya kurejea Ufaransa kuaga katika timu yake ya zamani, Nantes inayoshiriki Ligue 1 na akaposti picha na ujumbe , 'Kwaheri ya mwisho'.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 alitarajiwa kurejea Wales kwa wakati kuanza mazoezi asubuhi ya jana, lakini ndege binafsi ya Piper Malibu aliyopanda ikapoteza mwelekeo na kuanguka karibu na Casquets, Alderney majira ya saa 2.30 usiku wa jana.
  Mashabiki wa Cardiff wamekwishaanza kuomboleza ingawa bado haijathibitishwa kama mchezaji huyo amefariki dunia.
  Mwenyekiti wa Cardiff City FC, Mehmet Dalman alisema kwamba alikuwa anafuatilia sana taarifa za Sala wakati mchezaji mwenzake wa zamani wa Guingamp, kiungo Lucas Deaux alipotweet: “Natumai kutoka ndani ya moyo wangu kabisa, hii si kweli,”.
  Akizungumza kutoka Argentina, baba yake Sala, Horacio alisema alishtushwa na habari hizo juu ya mwanawe, ambaye aliongea naye mara ya mwisho Jumapili.
  Dereva huyo wa gari kubwa aina ya lori aliangua kilio huku akimuelezea mwanawe huyo kama 'kijana mdogo jasiri', 'Siwezi kuamini.'  
  Mama wa mchezaji huyo, Mercedes Taffarel amesema kwamba ndege hiyo mali ya Cardiff City, na  Emiliano alikuwa kwenye kipindi kizuri katika maisha yake kwa sasa.
  Afisa Mkuu wa kisiwa cha Channel, John Fitzgerald alisema kwamba kuna asilimia tano tu ya kumpata Sala na rubani wake. “Maji yalikuwa baridi mno wakati huo, hivyo kama kulikuwa kuna watu kwenye maji na kwa ubaridi wake wangeweza kudumu kwa saa moja tu kwa majira haya ya mwaka,”alisema.
  Ndege ya Piper Malibu iliruka umbali wa futi 2,300 na kupoteza mwelekeo angani kabla ya kuanguka.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: 'SELFIE' YAMTIA LAWAMANI RONALDO HAKUJALI KUHUSU SALA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top