• HABARI MPYA

  Ijumaa, Januari 18, 2019

  BUNDESLIGA YAREJEA, BORUSSIA DORTMUND WAIFUATA RB LEIPZIG

  BAADA ya mapumziko ya Siku kuu ni muda wa mzunguko wa pili wa ligi ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga, mzunguko wa pili ama hatua ya lala salama ni nafasi kwa timu zilizofanya vibaya mzunguko wa kwanza kupindua matokeo, na kwa zile zilizofanya vizuri kuendelea kujiimarisha zaidi.
  Ijumaa hii, Bayern Munich ambao hawakufanya vizuri sana mzunguko wa kwanza wana nafasi ya kusahihisha makosa na kuanza kuwafukuzia Borussia Dortmund wanaoongoza ligi kwa sasa. Bayern Munich watakuwa ugenini kwa Hoffeiheim kwenye mchezo utakaopigwa saa 4:30 Usiku majira ya Afrika Mashariki na kuonyeshwa Mubashara kupitia ST World Football.
  Mchezo mkubwa wikendi hii unatarajiwa kuwa ule wa RB Leipzig dhidi ya vinara Borussia Dortmund. Leipzig watakuwa nyumbani katika dimba la Red Bull Arena kukabiliana Dortmund wamepoteza mchezo mmoja tu hadi sasa. Mechi hiyo itachezwa siku ya Jumamosi saa 2:30 Usiku na kuonyeshwa moja kwa moja kupitia ST World Football pekee. 


  Kocha wa Dortmund Lucian Fevre huenda anasema nyota wake Marco Reus na kinara wa magoli Bundesliga Paco Alcacer wako fiti kucheza mchezo wa jumamosi. Reus alikuwa anasumbuliwa na tumbo, huku Alcacer akisumbuliwa na maumivu ya nyama za paja. 
  Kwa upande wa RB Leipzig wao wako vizuri na watawategemea zaidi Timo Werner mwenye kasi zaidi na Mshambuliaji wa Denmark mwenye asili ya Tanzania, Yussuf Poulsen ambaye ana nguvu za kutosha kuwasumbua mabeki wa kati wa Dortmund Dani Axel Zagadou na Manuel Akanji.
  Bayer Leverkusen watawakaribisha Borussia Mochengladbach jumamosi saa 11:30 jioni na mchezo utakuwa LIVE kupitia ST World Football. Wapenzi wa Soka nchini wataweza kutazama mechi hizi kupitia StarTimes pekee kwa kulipia kifurushi cha MAMBO Tsh 14,000 (watumiaji wa Antenna) na SMART Tsh 21,000 (watumiaji wa Dish) 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BUNDESLIGA YAREJEA, BORUSSIA DORTMUND WAIFUATA RB LEIPZIG Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top