Kikosi cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania Bara, kabla ya mchezo wa Kundi A, Kombe la Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge dhidi ya Zambia mjini Nairobi, Kenya Novemba 6, mwaka 1979 ambao ulimalizika kwa sare ya 2-2, mabao ya Kilimanjaro Stars yakifungwa na Mohamed Salim na Omar Hussein ‘Keegan’. Kutoka kulia waliosimama ni Salim Amir, Jellah Mtagwa, Athumani Mambosasa (sasa marehemu), Juma Mkambi ‘Jenerali’ (sasa marehemu), Mohamed Salim, Augustino Peter ‘Tino’ na kocha, Joel Bendera (sasa marehemu). Waliochuchumaa kutoka kulia ni Daudi Salum ‘Bruce Lee’, Omar Hussein ‘Keegan’, Mohammed ‘Adolph’ Rishard, Hussein Ngulungu na Mohamed Kajole (sasa marehemu). Siku hiyo, Nahodha Leodegar Tenga alianzia benchi na Salim Amir akacheza beki ya kati pamoja na Jellah Mtagwa.
Van Dijk sends Champions League warning to Real Madrid
-
Liverpool defender Virgil van Dijk has sent a warning to Real Madrid ahead
of the Champions League final on Saturday. Liverpool are looking for
revenge aft...
Dakika 15 zilizopita
0 maoni:
Chapisha Maoni