• HABARI MPYA

    Sunday, January 27, 2019

    SAMATTA ACHEZA HADI MWISHO KRC GENK YAGONGWA 2-1 NYUMBANI

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku wa jana amecheza kwa dakika zote 90, klabu yake, KRC Genk ikichapwa 2-1 na Royal Excel Mouscron nyumbani katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk.
    Lakini pamoja kichapo hicho, Genk inaongoza Ligi hiyo kwa pointi zake 51, ikifuatiwa na Antwerp yenye point 42 baada ya wote kucheza mechi 23 na Club Brugge pointi 41 za mechi 22, wakati Royal Excel Mouscron inainuka kutoka nafasi ya 15 hadi ya 12 kwenye ligi ya timu 16, sasa ikifikisha pointi 23 katika mechi ya 23.
    Katika mchezo wa jana, mabao ya Royal Excel Mouscron yalifungwa na M'Baye Leye kwa penalti dakika ya 17 na Taiwo Michael Awoniyi dakika ya  90 akimalizia pasi ya Nikola Gulan, wakati la Genk lilifungwa na S. Dewaest dakika ya 73, akimalizia pasi ya Bryan Heynen.

    Beki Mcameroon, Frank Boya wa Royal Excel Mouscron akiteleza mbele ya mshambuliaji Mtanzania wa KRC Genk, Mbwana Samatta kuondoa mpira jana Uwanja wa Luminus Arena 

    Kwa Samatta mwenye umri wa miaka 26, jana amefikisha jumla ya mechi 139 za mashindano yote alizoichezea KRC Genk tangu amejiunga nayo Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) akiwa amefunga mabao 55.
    Kwenye Ligi ya Ubelgiji pekee amecheza mechi 107 na kufunga mabao 40, wakati Europa League amefunga mabao 14 katika mechi 22 na katika Kombe la Ubelgiji amefunga mabao mawili katika mechi tisa.
    Kikosi cha KRC Genk kilikuwa: Jackers, Maehle, Aidoo, Dewaest, Borges, Heynen, Wouters/Fiolic dk46, Malinovskyi, Ndongala/Gano dk47, Trossard na Samatta.
    RE Mouscron; Butez, Dussenne, Friede, Awoniyi, Boya, Leye, Bakic, Gulan, Vojvoda, Vandurmen/Pierrot dk81 na Godeau.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SAMATTA ACHEZA HADI MWISHO KRC GENK YAGONGWA 2-1 NYUMBANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top