• HABARI MPYA

    Monday, January 21, 2019

    STEVEN PIENAAR ALIYEWIKA EVERTON AJA DAR WIKI KUFANYA MAZOEZI NA SERENGETI BOYS

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KIUNGO wa zamani wa timu ya Everton FC na Balozi  wa klabu hiyo, Steven Pienaar anatarajiwa kutua mjini Dar es Salaam wiki hii.
    Pienaar, nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Afrika Kusini, Bafana Bafana katika ziara yake hiyo atafanya mazoezi na timu ya taifa ya ya vijana chini ya umri wa miaka, Serengeti Boys inayojiandaa na Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) U17, michuano itakayofanyika baadaye mwaka huu.
    Pamoja na hayo, Pienaar atawatia hamasa wachezaji chipukizi hapa nchini wa klabi ya Bom Bom FC.
    Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti SportPesa Tanzania Tarimba Abbas alisema kuwa ziara ya Steven Pienaar hapa nchini ni moja ya mikakati ya muda mrefu ya SportPesa ya kukuza mpira wa miguu hapa Tanzania.
    Gwiji wa Afrika Kusini, Steven Pienaar anatarajiwa kutua mjini Dar es Salaam wiki hii

    Kwa muda mrefu SportPesa imekuwa na mikakati dhabiti ya kukuza mpira wa soka hapa nchini na kwa sababu ndio imeifanya timu ya Everton FC kwa kushirikiana na SportPesa imeamua mchezaji huyo anafanya ziara hapa nchini. Huyu ni Mwafrika mwenzetu ambaye alikuwa na wakati mzuri wakati alipokuwa akiichezea timu ya Everton FC na kwa sasa ni mmoja ya Balozi wa timu hiyo. Ziara yake pamoja na kufanya mazoezi na timu ya U17 itakuwa na hamasa kubwa na hasa kwa wakati huu ambapo timu hiyo inajiandaa na michuano ya AFCON ambayo itachezwa kwenye uwanja wa Taifa wa Dar es Salaam. SportPesa itaendelea kushirikiana na serikali pamoja na wadau wengi kwenye mikakati ya kukuza soka hapa nchini, alisema Abbas.
    TIMU zinazoshiriki michuano ya SportPesa Cup zilianza kuingia Dar es Salaam mwishoni mwa wiki huku michuano hiyo ikitarajiwa kutimua vumbi wiki hii. Michuano hiyo ambayo imekuwa ikifuata umati mkubwa wa mashabiki ukanda huu wa Afrika Mashariki wiki itashuhudia timu 8 zikishiriki, huku Kenya na Tanzania kila moja ikiwakilishwa na timu nne
    Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti SportPesa Tanzania Tarimba Abbas alisema kuwa matayarisho ya michuano hiyo awamu ya tatu yamekamilika huku zikiwa zimeanza kuingia Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. SportPesa Cup awamu ya tatu inatarajiwa kuanza Jumanne ya wiki hii. Timu zilishiriki kutoka Kenya zilianza kufika jijini Dar es Salaam mnamo Jumamosi. Ni matarajio yetu kwamba mpaka Jumatatu timu zote zitakuwa zimefika. Natoa wito kwa mashabiki wa soka kujitokeza kwa wingi kushuhudia michuano hii kwani tumeyaboresha ili yazidi kuwa bora zaidi, alisema Abbas.
    Abbas alisema kuwa SportPesa kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) wamekubaliana kutoza kiingilio cha chini ili kuweza kuvutia mashabiki wengi. Mashabiki wa mpira wa miguu kutoka Tanzania na Ukanda huu wa Afrika Mashariki kwa jumla watalipa TZS 10,000 kwa VIP A,huku VIP B na VIP C wakilipa TZS 5,000 na mzunguko TZS 2,000 kwa mechgi za robo fainali. Nia yetu ni kuweza kufanya mashabiki wa michuano ya SportPesa Cup kujisikia wamedhaniwa na hivyo nawaomba wajitokeze kwa wingi kushangilia timu zao kwani bingwa wa michuano hii atacheza mechi ya kirafiki na moja timu inayoshiriki Ligi Kuu nchini Uingereza ya Everton FC.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: STEVEN PIENAAR ALIYEWIKA EVERTON AJA DAR WIKI KUFANYA MAZOEZI NA SERENGETI BOYS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top