Lionel Messi akishangilia baada ya kuifungia Barcelona bao la tatu dakika ya 90 na ushei katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Leganes kwenye mchezo wa La Liga usiku wa jana Uwanja wa Camp Nou, hilo likiwa bao la 25 kwa Muargentina huyo katika mechi 24 za mashindano yote msimu huu. Mabao mengine ya Barca yamefungwa na Ousmane Dembele dakika ya 32 na Luis Suarez dakika ya 71 na kwa ushindi huo, timu hiyo ya Katalunya inafikisha pointi 46 baada ya kucheza mechi 20 ikiendelea kuongoza La Liga kwa pointi tano zaidi ya Atlético Madrid wanaofuatia nafasi ya pili na 10 zaidi ya Real Madrid walio nafasi ya tatu PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Arsenal fans fume as Man City's Rodri catches Martin Odegaard with a horror tackle
-
Arsenal fans have been left fuming after Man City midfielder Rodri left
Martin Odegaard in agony after a crunching challenge on Saturday.
30 minutes ago
0 comments:
Post a Comment