• HABARI MPYA

    Tuesday, January 15, 2019

    NDEMLA AWASILI SALAMA SWEDEN, KUANZA MAJARIBIO KESHO AFC ESKILSTUNA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KIUNGO chipukizi wa kimataifa wa Tanzania, Said Hamisi Ndemla kesho anatarajiwa kuanza majaribio mafupi katika klabu ya AFC  Eskilstuna ya Ligi Kuu ya Sweden.
    Hiyo ni baada ya mchezaji huyo wa Simba SC kuwasili salama mjini Stockholm jana akitokea Dar es Salaam akiwa ameongozana na mshambuliaji mwingine chipukizi wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Rashid Chambo wa JKT Ruvu.
    Meneja wa mchezaji huyo, Said Suleiman Sharrif ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online leo kwamba wawili hao wataanza majaribio ya kesho baada ya kupumzika leo.
    Said Ndemla (kulia) akiwa na Meneja wake, Said Suleiman Sharrif baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Stokholm jana
    Said Ndemla (kulia) akiwa na Meneja wake, Said Suleiman Sharrif na mchezaji mwenzake, Rashid Chambo baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Stockholm jana  

    Ndemla mwenye umri wa miaka 22, alifuzu majaribio katika klabu hiyo Novemba mwaka juzi (2017) chini ya kocha Muingereza Michael Jolley, lakini akasaini mkataba mpya kuendelea kuichezea Simba na kuachana na ofa hiyo.
    Ila sasa, Simba baada ya kupata viungo wengine bora kama Hassan Dilunga na Mzambia Clatous Chama wapo tayari kumuachia Ndemla na kijana huyo amekwenda kujaribu tena bahati yake chini ya kocha mpya, Nemanja Miljanovic.
    Miljanovic amesema japokuwa Ndemla alifuzu majaribio Novemba mwaka 2017, lakini atahitaji kujiridhisha juu ya uwezo wake kwa majaribio mafupi tu wiki hii.
    Chambo yeye atapewa wiki wiki mbili za majaribio katika klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya Sweden ijulikanayo kama Allsvenskan.
    Said Ndemla (kulia) akiwa kwenye ndege na mchezaji mwenzake, Rashid Chambo wakati wa safari ya Sweden jana
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NDEMLA AWASILI SALAMA SWEDEN, KUANZA MAJARIBIO KESHO AFC ESKILSTUNA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top