• HABARI MPYA

  Saturday, January 19, 2019

  AZAM FC YAIPIGA 1-0 MWADUI NA KUFUFUA MATUMAINI YA UBINGWA LIGI KUU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  AZAM FC imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Mwadui FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku wa leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Ushindi huo umetokana na bao pekee la mshambuliaji Mzimbabwe, Donald Ngoma dakika ya 70 katika mchezo uliokuwa mkali na wa kusisimua.
  Azam FC inafikisha pointi 44 baada ya ushindi huo katika mechi ya 19 ya msimu, sasa ikizidiwa pointi tisa tu na vinara, Yanga SC ambao hata hivyo wamecheza mechi moja zaidi, wakati mabingwa watetezi, Simba SC wana pointi 33 za mechi 14.

  Mapema katika mchezo uliotangulia leo jioni, Yanga SC ilipoteza mechi ya kwanza ya msimu wa Ligi Kuu baada ya kuchapwa bao 1-0 na wenyeji, Stand United Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga.
  Safari ya kucheza bila kufungwa kwa Yanga katika msimu imeishia katika mechi ya 20 na sasa wanabaki na pointi zao 53, ingawa wanaendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi tisa zaidi ya Azam FC wanaofuatia katika nafasi ya pili.
  Bao lililoizamisha Yanga SC limefungwa na  Nahodha wa Stand United, Jacok Massawe dakika ya 88 akimtungua kwa kichwa kipa Klaus Kindoki kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kufuatia krosi ya Mwinyi Elias kutoa upande wa kulia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAIPIGA 1-0 MWADUI NA KUFUFUA MATUMAINI YA UBINGWA LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top