• HABARI MPYA

  Jumamosi, Januari 26, 2019

  BALOTELLI AANZA NA BAO MARSEILLE IKICHAPWA 2-1 NA LILLE

  Mshambuliaji Mtaliano, Mario Balotelli akishangilia baada ya kuifungia timu yake mpya, Marseille bao la kufutia machozi dakika ya 90 na ushei katika mchezo wake wa kwanza baada ya kujiunga nayo wiki hii akitokea Nice ikifungwa 2-1 na Lille usiku wa jana Uwanja wa Orange Velodrome mjini Marseille.
  Mabao ya Lille yote yalifungwa na Nicolas Pepe dakika za 45 na ushei kwa penalti na 90 na ushei, dakika mbili kabla ya bao la Balotelli aliyetokea benchi dakika ya 74 kuchukua nafasi ya Boubacar Kamara kufuatia kuvunja mkataba na Nice Januari 23 mwaka huu na kusaini mkataba wa hadi mwishoni mwa msimu na Marseille 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BALOTELLI AANZA NA BAO MARSEILLE IKICHAPWA 2-1 NA LILLE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top