• HABARI MPYA

  Jumatano, Januari 30, 2019

  MAN CITY WAGONGWA 2-1 NA NEWCASTLE UNITED ST JAMES' PARK

  Mshambuliaji wa kimataifa wa Scotland, Matt Ritchie akikimbia kushangilia baada ya kuifungia Newcastle United bao la ushindi kwa penalti dakika ya 80 kufuatia Fernandinho kumchezea rafu Sean Longstaff katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Manchester City kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa jana Uwanja wa St. James' Park. Manchester City walitangulia kwa bao la Sergio Aguero dakika ya kwanza tu kabla ya Newcastle kusawazisha kupitia kwa Salomon Rondon dakika ya 66.
  Man City inazidi kuuweka rehani ubingwa wa Ligi Kuu England, sasa wakibaki na pointi zao 56 baada ya kucheza mechi 23, moja zaidi ya vinara Liverpool wanaoongoza kwa pointi zao 60, wakati Newcastle sasa wanafikisha pointi 24 katika mechi 24, wakipanda hadi nafasi ya 14 kutoka ya 17 kwenye ligi ya timu 20 
    
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAN CITY WAGONGWA 2-1 NA NEWCASTLE UNITED ST JAMES' PARK Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top