• HABARI MPYA

  Jumanne, Januari 22, 2019

  YANGA SC, SINGIDA UNITED ZATUPWA NJE MAPEMA MICHUANO YA SPORTPESA

  Na Sada Salmin, DAR ES SALAAM
  YANGA SC imeendeleza rekodi yake ya kufanya vibaya kwenye michuano ya SportPesa Super Cup baada ya leo kuchapwa mabao 3-2 na Kariobangi Sharks ya Kenya na kutupwa nje katika Raundi ya kwanza tu.
  Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam, kipa Klaus Kindoki aliwaruhusu Kariobangi Sharks kwenda kupumzika wakiwa wanaongoza mabao 2-0.
  Mabao hayo yalifungwa na Abuye Duke dakika ya 10 kwa shuti kali akitumia uzembe wa mabeki wa Yanga na Abege George dakika ya 36 akiunganisha pasi ya Patilan Omotto.
  Kipindi cha pili baada ya mawaidha ya kocha wao, Mwinyi Zahera raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Yanga kidogo wakabadilika na kufanikiwa kupata mabao mawili, ingawa pia waliruhusu bao lingine moja.
  Nahodha wa Yanga, Ibrahim Ajibu akitafuta maarifa ya kumpita mchezaji wa Kariobangi Sharks
  Kikosi cha Yanga kabla ya mchezo na Kariobangi Sharks leo Uwanja wa Taifa
  Kikosi cha Kariobangi Sharks kabla ya mchezo na Yanga  leo Uwanja wa Taifa

  Mshambuliaji Mrundi, Amissi Joselyn Tambwe alimtoka kipa wa Sharks na kuifungia Yanga bao la kwanza katika dakika 86 baada ya kupokea pasi ya kiungo Mkongo, Papy Kabamba Tshishimbi.
  Wakati Yanga wakisaka mabao zaidi wakajikuta wanapachikwa wao bao la tatu, mfungaji Abuya Duke dakika ya 90 baada ya kuwachambua mabeki wa Yanga na kupiga shuti lililomshinda Kindoki.
  Wachezaji wa Yanga walifuata mpira golini ili kuanza lakini kipa wa Sharks aliung'ang'ania jambo lilosababisha kumpokonya kwa nguvu na wachezaji wa Sharks kuja ambapo ikasababisha kupigana
  Ugomvi hup ulidumu kwa dakika sita baada ya waamuzi watatu kutuliza vurugu ndani, mpira ukaendelea na Yanga wakapata bao la pili katika dakika ya 90, mfungaji mshambuliaji Mkongo, Heritier Makambo akiunganisha krosi ya Nahodha, Ibrahim Ajibu.
  Katika mchezo uliotangulia mchana wa leo, Singida United nayo ilitupwa nje ya michuano hiyo baada ya kuchapwa 1-0 na Bandari ya Kenya. 
  Michuano hiyo itaendelea kesho kwa mechi nyingine mbili baina ya timu za Tanzania na Kenya, kwanza Mbao FC wakimenyana na Gor Mahia kuanzia Saa 8:15 mchana na baadaye Simba SC wakiikabili AFC Leopards Saa 10:15. 
  Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Klaus Kindoki, Paul Godfrey/Juma Abdul dk81, Gardiel Michael, Andrew Vincent ‘Dante’, Abdallah Shaibu ‘Ninja’/Thabani Kamusoko dk46, Ibrahim Ajibu, Feisal Salum/Papy Kabamba Tshishimbi dk84, Heritier Makambo, Haruna Moshi/Amis Tambwe dk46 na Mrisho Ngassa/Deus  Kaseke dk54.
  Kariobangi Sharks: Onyemba John, Lemu Geoffrey, Keta Thomas, Bodo Michael, Omondi Nison, Patilan Omotto, Abuya Duke, Vincent Wasambo/ Oyudi Shaphan dk63, Vidah Sven, Mwendwa Harrison/Juma Eric dk71 na Abege George/John Kuol dk76.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA SC, SINGIDA UNITED ZATUPWA NJE MAPEMA MICHUANO YA SPORTPESA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top