• HABARI MPYA

  Alhamisi, Januari 31, 2019

  CHELSEA YAFUMULIWA 4-0 NA BOURNEMOUTH NA KUONDOLEWA 'TOP FOUR

  Mshambuliaji wa AFC Bournemouth, Joshua King akishangilia baada ya kuifungia mabao mawili timu yake dakika za 47 na 74 katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Chelsea kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Vitality mjini Bournemouth, Dorset. Mabao mengine ya Bournemouth yamefungwa na David Brooks dakika ya 63 na Charlie Daniels dakika ya 90 na ushei katika siku ambayo mchezaji mpya Gonzalo Higuain alianza vibaya urejeo wake ligi ya England klabu ya Chelsea ikipigwa na kutolewa kwenye nne Bora ya msimamo wa ligi.
  Kipigo hicho kinaifanya Chelsea sasa ilingane kwa kila kitu na Arsenal, idadi ya mechi za kucheza wote 24, wastani wa mabao wote jumlisha 17 na pointi wote 47, wakati Bournemouth inafikisha pointi 33 katika mechi ya 24 na kupanda kutoka nafasi ya 12 hadi ya 10 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CHELSEA YAFUMULIWA 4-0 NA BOURNEMOUTH NA KUONDOLEWA 'TOP FOUR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top