• HABARI MPYA

  Tuesday, January 29, 2019

  NAPOLI MIKONONI MWA AC MILAN, JUVE KWA ATALANTA COPPA ITALIA

  ROBO fainali ya Coppa Italia msimu huu imekaa kama shindano la 8 bora ya Serie A ambapo Fiorentina timu pekee nje ya nane bora katika msimamo wa ligi ya Serie A msimu huu.
  Shughuli inaanzia jijini Milan ambapo wenyeji AC Milan watawakaribisha Napoli katika dimba la San Siro saa 4:45 Usiku. Napoli inashika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi ya Serie A nyuma ya Juventus ambao wamezidi wamezidi kuimarika siku za hivi karibuni. Licha ya Napoli kuwa na kikoso kizuri bado hawajaweza kushindana na Juventus, na Kombe la Coppa Italia ndio nafasi yao wazi zaidi kushinda taji mwaka huu japo haitakuwa rahisi.
  AC Milan wao wana muda mrefu zaidi wakiwa hawajashinda Kombe japo walishinda taji la Super Coppa Italiana mwaka 2016 huku wakiwa hawajashinda ligi wa Kombe la Shirikisho. Wenzao Inter Milan watakuwa nyumbani pia dhidi ya Lazio siku ya Alhamisi saa 5:00 Usiku.Kesho Jumatano, Fiorentina watakuwa nyumbani dhidi ya Roma na mechi itachezwa saa 2:15 Usiku kwa saa za Afrika mashariki. 
  Cristiano Ronaldo aliwapatia Juventus ushindi katika Supercoppa dhidi ya Milan wiki mbili zilizopita na Dybala kumwagia sifa kibao baada ya mechi
  “Tunafahamu umuhimu wa Cristiano Ronaldo na ukubwa wa mchango wake kila siku. Mara zote nimekuwa nikisema yeye na Messi wako kwenye kiwango sawa. Mimi nina bahati ya kucheza nao wote”
  Juventus watakuwa ugenini dhidi ya Atalanta siku ya Jumatano saa 4:45 Usiku na michezo yote hii itakuwa MUBASHARA kupitia ST World Football pekee.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NAPOLI MIKONONI MWA AC MILAN, JUVE KWA ATALANTA COPPA ITALIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top