• HABARI MPYA

  Friday, January 25, 2019

  AZAM FC YAIPIGA BIASHARA UNITED 2-1 NA KUIKARIBIA YANGA KILELENI LIGI KUU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Azam FC imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Biashara United ya Mara katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam.
  Ushindi huo unaifanya Azam FC ifikishe pointi  47 baada ya kucheza mechi, sasa ikizidiwa pointi sita tu na vinara, Yanga SC wanaoongoza ligi hiyo kwa pointi zao, 53 za mechi 20 pia, wakiwazidi kwa pointi 20 mabingwa watetezi, Simba SC ambao hata hivyo wamecheza mechi 14.
  Haukuwa ushindi mwepesi kwa Azam FC leo, kwani ililazimika kutoka nyuma baada ya kutanguliwa kwa bao la mapema la Daniel Manyenye dakika ya pili.

  Azam FC ilisawazisha bao kupitia kwa kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’ dakika ya 46, kabla ya Ramadhani Singano ‘Messi’ kufunga la ushindi dakika ya 62.
  Kwa kipigo hicho, Biashara United inabaki nafasi ya 18 kwenye Ligi Kuu ya timu 20, ikiwa na pointi 20 mbele ya African Lyon yenye pointi 19 za mechi 23 na Tanzania Prisons pointi 17 za mechi 22.
  Mechi nyingine ya Ligi Kuu iliyochezwa leo jioni Uwanja wa Meja Isamuhyo huko Mbweni, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, wenyeji JKT Tanzania wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Mtibwa Sugar ya Morogoro.
  Matokeo hayo yanayoifanya kila timu ijiongezee pointi moja, yanaifanya Mtibwa Sugar ifikishe pointi 27 baada ya kucheza mechi 19 ikibaki nafasi ya 10 na JKT inafikisha pointi 26 katika mechi 23 na kuendelea kushika nafasi ya 12.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAIPIGA BIASHARA UNITED 2-1 NA KUIKARIBIA YANGA KILELENI LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top