• HABARI MPYA

  Jumatatu, Januari 21, 2019

  KUMEKUCHA MICHUANO YA SPORTPESA CUP 2019, KIPUTE KUANZA JUMANNE DAR

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU zinazoshiriki michuano ya SportPesa Cup zilianza kuingia Dar es Salaam mwishoni mwa wiki huku michuano hiyo ikitarajiwa kutimua vumbi wiki hii. 
  Michuano hiyo ambayo imekuwa ikifuata umati mkubwa wa mashabiki ukanda huu wa Afrika Mashariki wiki itashuhudia timu 8 zikishiriki, huku Kenya na Tanzania kila moja ikiwakilishwa na timu nne
  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti SportPesa Tanzania Tarimba Abbas alisema kuwa matayarisho ya michuano hiyo awamu ya tatu yamekamilika huku zikiwa zimeanza kuingia Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
  Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti SportPesa Tanzania Tarimba Abbas akizungumza na Waandishi wa Habari leo mjini Dar es Salaam

  SportPesa Cup awamu ya tatu inatarajiwa kuanza Jumanne ya wiki hii. Timu zilishiriki kutoka Kenya zilianza kufika jijini Dar es Salaam mnamo Jumamosi. 
  Ni matarajio yetu kwamba mpaka Jumatatu timu zote zitakuwa zimefika. Natoa wito kwa mashabiki wa soka kujitokeza kwa wingi kushuhudia michuano hii kwani tumeyaboresha ili yazidi kuwa bora zaidi, alisema Abbas.
  Abbas alisema kuwa SportPesa kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) wamekubaliana kutoza kiingilio cha chini ili kuweza kuvutia mashabiki wengi. 
  Mashabiki wa mpira wa miguu kutoka Tanzania na Ukanda huu wa Afrika Mashariki kwa jumla watalipa TZS 10,000 kwa VIP A, huku VIP B na VIP C wakilipa TZS 5,000 na mzunguko TZS 2,000 kwa mechgi za robo fainali. 
  Nia yetu ni kuweza kufanya mashabiki wa michuano ya SportPesa Cup kujisikia wamedhaniwa na hivyo nawaomba wajitokeze kwa wingi kushangilia timu zao kwani bingwa wa michuano hii atacheza mechi ya kirafiki na moja timu inayoshiriki Ligi Kuu nchini Uingereza ya Everton FC.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KUMEKUCHA MICHUANO YA SPORTPESA CUP 2019, KIPUTE KUANZA JUMANNE DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top